Chama cha Wanachuo

Chuo kina chama cha wanachuo kinachotambulika kama MeSo (Meteorological Students’ Organization) ambacho kinaunganisha mawasiliano baina ya wanachuo na utawala. Mwanachuo aliyesajiliwa na chuo ni mwanachama wa MeSO. Uchaguzi wa kidemokrasia hufanyika kila mwaka kulingana na katiba ya MeSO.