Habari

Imewekwa: 25/03/2019

Chuo chaadhimisha siku ya hali ya hewa duniani

Chuo chaadhimisha siku ya hali ya hewa duniani

Chuo Cha Taifa cha Hali ya Hewa kikishirikiana na kituo cha hali ya hewa Kigoma Airport chaadhimisha siku ya hali ya hewa duniani 23 Machi 2019.

Wakufunzi na wafanyakazi wa kituo cha hali ya hewa Kigoma wamekutana na wanafunzi mbalimbali pamoja na wananchi waliotembelea kituoni hapo na kuwapatia mafunzo mbalimbali yanayohusiana na masuala ya hali ya hewa kwa kuzingatia zaidi kauli mbiu ya mwaka huu ya Jua, Dunia na Hali ya hewa.